Imperial College of Health And Allied Sciences

- (ICHAS) -

News & Events

01
Jul 2026

September 2026 Admissions Now Open - ICHAS

IMPERIAL COLLEGE OF HEALTH AND ALLIED SCIENCES (ICHAS) is pleased to announce that applications are now open for the September 2026 Intake. If you aspire to build a rewarding career in the healthcare profession, this is your opportunity to study at one of Zanzibar's growing health training institutions committed to academic excellence, practical skills, and professional integrity. Our programmes are designed to prepare competent healthcare professionals who are ready to serve communities both nationally and internationally through quality education, modern training facilities, and experienced academic staff. Programmes Offered 1. Ordinary Diploma in Clinical Dentistry (3 Years) This programme prepares students to become competent oral healthcare professionals with practical knowledge and clinical skills in preventive, restorative, and community dental care. Entry Qualifications Applicants must possess a Certificate of Secondary Education Examination (CSEE) with at least four (4) passes in non-religious subjects, including: Biology Chemistry Physics or Engineering Science 2. Ordinary Diploma in Nursing and Midwifery (3 Years) Train to become a compassionate and highly skilled nurse capable of providing quality healthcare services in hospitals, clinics, and community settings. Entry Qualifications Applicants must possess a Certificate of Secondary Education Examination (CSEE) with: At least four (4) passed subjects A minimum grade of C in Biology A minimum grade of C in Chemistry A pass in Physics/Engineering Science A pass in English Language A pass in Mathematics is an added advantage. 3. Ordinary Diploma in Pharmaceutical Sciences (3 Years) Develop the knowledge and practical competencies required to become a pharmaceutical professional involved in medicine preparation, dispensing, storage, and patient care. Entry Qualifications Applicants must possess a Certificate of Secondary Education Examination (CSEE) with at least five (5) passes in: Biology Chemistry Physics Mathematics English Language Why Choose ICHAS? At ICHAS, students benefit from: Quality health sciences education Experienced and qualified lecturers Modern practical and clinical training Competency-based learning Supportive learning environment Career-focused programmes that prepare graduates for employment and professional growth September 2026 Intake is Now Open Applications are currently being received for all three diploma programmes. Prospective students who meet the admission requirements are encouraged to submit their applications early to secure their place before the intake closes. Start your journey towards a respected and fulfilling healthcare career today. For applications, contact: 0778 454 565 or email: info@ichas.ac.tz or you can apply directly via www.maombi.ichas.ac.tz

Dirisha l ........

Soma Zaidi
01
Jul 2026

Udahili wa Septemba 2026 Umefunguliwa - (ICHAS)

IMPERIAL COLLEGE OF HEALTH AND ALLIED SCIENCES (ICHAS) inawatangazia wanafunzi wote waliomaliza elimu ya sekondari kuwa maombi ya kujiunga na masomo kwa muhula wa Septemba 2026 yamefunguliwa rasmi. Ikiwa unatamani kujenga taaluma yenye heshima na mchango mkubwa katika jamii kupitia sekta ya afya, huu ndio wakati wako wa kuchukua hatua. ICHAS imejizatiti kutoa elimu bora inayozingatia umahiri, maadili ya taaluma, pamoja na mafunzo ya vitendo yanayowaandaa wahitimu kuwa wataalamu wenye uwezo wa kufanya kazi katika vituo mbalimbali vya afya nchini na nje ya nchi. Kozi Zinazotolewa 1. Stashahada ya Kawaida ya Udaktari wa Meno (Ordinary Diploma in Clinical Dentistry) – Miaka 3 Kozi hii inawaandaa wanafunzi kuwa wataalamu wa afya ya kinywa na meno wenye uwezo wa kutoa huduma za kinga, matibabu na ushauri wa afya ya meno kwa viwango vya kitaaluma. Sifa za Kujiunga Mwombaji anatakiwa kuwa na Cheti cha Kidato cha Nne (CSEE) chenye angalau ufaulu wa masomo manne (4) yasiyo ya dini, yakiwemo: Baiolojia (Biology) Kemia (Chemistry) Fizikia (Physics) au Engineering Science 2. Stashahada ya Kawaida ya Uuguzi na Ukunga (Ordinary Diploma in Nursing and Midwifery) – Miaka 3 Kozi hii inawaandaa wanafunzi kuwa wauguzi na wakunga wenye ujuzi wa kutoa huduma bora za afya kwa wagonjwa, familia na jamii kwa ujumla. Sifa za Kujiunga Mwombaji anatakiwa kuwa na Cheti cha Kidato cha Nne (CSEE) chenye: Angalau masomo manne (4) yaliyofaulu Daraja la C au zaidi katika Baiolojia Daraja la C au zaidi katika Kemia Ufaulu katika Fizikia (Physics) au Engineering Science Ufaulu katika Lugha ya Kiingereza (English Language) Kupata ufaulu katika Hisabati ni faida ya ziada. 3. Stashahada ya Kawaida ya Sayansi ya Famasia (Ordinary Diploma in Pharmaceutical Sciences) – Miaka 3 Kozi hii inawawezesha wanafunzi kupata maarifa na ujuzi wa kitaaluma katika utayarishaji, uhifadhi, usambazaji na matumizi sahihi ya dawa pamoja na huduma kwa wagonjwa. Sifa za Kujiunga Mwombaji anatakiwa kuwa na Cheti cha Kidato cha Nne (CSEE) chenye angalau ufaulu wa masomo matano (5) yafuatayo: Baiolojia (Biology) Kemia (Chemistry) Fizikia (Physics) Hisabati (Mathematics) Lugha ya Kiingereza (English Language) Kwa Nini Uchague ICHAS? Kwa kujiunga na ICHAS utapata: Elimu bora inayokidhi viwango vya taaluma za afya. Wahadhiri wenye uzoefu na weledi wa hali ya juu. Mafunzo ya vitendo yanayokuandaa kwa mazingira halisi ya kazi. Mazingira rafiki ya kujifunzia. Fursa ya kujenga taaluma yenye heshima na mahitaji makubwa katika sekta ya afya. Udahili wa Septemba 2026 Unaendelea Usikose nafasi ya kutimiza ndoto zako za kuwa mtaalamu wa afya. Tunawahimiza waombaji wote wenye sifa kuwasilisha maombi yao mapema ili kujihakikishia nafasi ya kujiunga na masomo. ICHAS – Tunakuandaa Leo, Uwe Mtaalamu wa Afya wa Kesho. Karibu Imperial College of Health and Allied Sciences (ICHAS), mahali ambapo ndoto zako za kuwa mtaalamu wa afya zinaanza kutimia. kwa maoambi, wasiliana nasi kwa namba : 0778 454 565 au baruapepe: info@ichas.ac.tz Au unaweza kutuma maombi moja kwa moja kupitia www.maombi.ichas.ac.tz

Dirisha l ........

Soma Zaidi
03
Jul 2026

ZHESLB - MWONGOZO WA UTOAJI MIKOPO KWA WAOMBAJI WAPYA WA NGAZI YA DIPLOMA KWA MWAKA WA MASOMO 2026/2027

Dirisha l ........

Soma Zaidi